OPINIONSPolitics

Kwa Nini “Yote Yawezekana Bila…” Utaimbiwa Ruto

Kenya imepitia vipindi tofatifauti vya kisiasa. Kila kipindi kimesheheni sifa muhimu na wanasiasa wenye mitazamo mbalimbali.

Katika mwaka wa 1963, Kenya ilipata uhuru kwa kijikomboa kutoka kwenye minyororo iliwekwa na Mashetani.

Katika mwaka uliofuata, Kenya ilipiga hatua na kupata Madaraka. Katika vipindi hivi, wanasiasa walioangaziwa sana walikuwa Hayati Jomo Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga, Ronald Ngala, miongoni mwa wengine.

Ukombozi wa pili ulifanyika mwaka wa 2002, pale ambapo utawala wa kiimla wa Mzee Daniel Moi, uliwekwa kikomo.

Vuguvugu la Rainbow, ukiongozwa na Mwai Kibaki, Raila Odinga, Kijana Wamalwa, Martha Karua, miongono mwa wengine, walihakikisha kwamba utawala wa miaka 24, ambao kwa mitazamo ya Waakenya wengi ulizima matumaini ya wengi, ulikatika.

Katika kipindi hiki, katika mwaka wa 2010, Kenya iliandika katika mpya. Katiba hii ilitilia mkazo maswala nyeti yakiwema Haki za Kimsingi za Wakenya, Ugatuzi, Utawala, Mamlaka za Viongozi.

Ukombozi wa tatu, na wa mwisho, kwa mujubu wa Raila Odinga, na hata pia wachambuzi wa maswala ya kisiasa, wakiwemi Herman Manyora, Mutahi Ngunyi na Profesa Adama Oloo, ni ule ya kiuchumi.

Sadfa

Kinachosadifisha ni kwamba, Rais Moi alipokuwa akiondoka mamlakani katika mwaka wa 2002, Wakenya kwa ghadhabu zao, walimtungia wimbo.

“Yote yawezekana kwa imani” ilibadilishwa kuwa “yote yawezekana bila Moi.

Kuimba huko kulikuwa rahisi kwa kuwa nomino au jina Moi lina sibali mbiliMo + i = Moi. Kulikuwa na mpigo, na urudiaji wake ulifana zaidi.

Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

Wimbo huu, hata hivyo, hukuimbwa katika miaka ya 2007, 2013 na 2017.

Sababu ni kwamba, katika mwaka wa 2007, kutokana na migogoro iliyotokana na madaiya wizi ya kura ya irais, aliyetangazwa mshindi Mwai Kibaki, hakuapishwa hadharani, bali kwa siri kwenye giza tororo, kwenye Ikulu, huko Nairobi.

Sababu ya pili; miaka ya 2013, na 2017, ‘ushindi’ wa Uhuru Kenyatta hukuwa wa wazi, wala wa ukweli. Isitoshe, mwaka wa 2017, kuteuliwa kwake kulifutitiwa mbali na Mahakama Makuu.

Tatu, na ya muhimu zaidi, wimbo huu ungeimbiwa nani? Ungeimbiwa Raila Odinga? Hungewezekana kwa kula hakungekuwa na mpigo wa sauti – wimbo huwengeimbika – kwa kuwa Raila ina silabi tatu – Ra+i+la. HUNGELETA SHANGWE!

Mwaka huu, Mheshimiwa William Ruto ataimbiwa wimbo huu kwa kuwa jina lake lina silabi mbili, ambazo zinaoana na mtindo na mdundo wa wimbo huu:  Ru+to = Ruto; “Yote yawezekana bila Ruto.”

Maajabu zaidi

Maajabu zaidi ni kuwa Rais Moi alikuwa anatoka katika jamii ya Wakalenjin, sawia na Bwana Ruto.

Katika mwaka wa 2002, Ruto alishirikiana zaidi na Rais Moi, ila Moi alikuwa anastaafu, huku Ruto akianza safari ya kujenga misingi dhabiti ya siasa zake.

Mwaka huu, Ruto ni naibu wake Rais Uhuru Kenyatta, ambaye atakuwa anaondoka mamlakani rasmi Agosti, baada ya kuaspishwa kwa rais wa tano. Kwa upande mwingine Ruto, kwa mara nyingine, atakuwa ananza misingi ya kuwa rais wa nchi ya Kenya.

Spread the love

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also
Close
Back to top button
error: Content is protected !!